SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Skin Goals Ni Ipi?
Urembo

Skin Goals Ni Ipi? 

Wakati tupo kwenye mitandao tunaweza kudanganyika na baadhi ya matangazo ambayo yanatuaminisha ngozi nzuri ni zile ambazo hazina kasoro, lakini kumbe kila mtu ana ngozi ya aina yake inawezekana kuna waliobarikiwa hawana madoa au vipele lakini pia ukiwa unavyo haimaanishi ngozi yako ni mbaya.

Lengo ni kuwa na ngozi yenye afya na sio perfect skin,

Je Ngozi yenye afya ni ipi?

  • Protected

Ngozi yenye afya ni ile ambayo inalindwa, kuanzia nje mpaka ndani hapa tukimaanisha unakula, kunywa vyakula ambavyo vinasaidia ngozi yako kuwa nzuri lakini pia vipodozi unavyopaka vinalinda ngozi yako badala ya kuiharibu bila kusahau kupaka sun screen ili kulinda ngozi yako kutokana na miale ya jua.

Umuhimu Wa Kupaka Sunscreen Katika Ngozi

  • Yenye Usawa ( Balanced )

Ngozi yenye afya ni ile ambayo inausawa, hapa hatuongelei tu kuhusu kuwa na rangi moja bali pia mafuta katika ngozi yako yapo sawa yaani hawajazidi wala kupungua, cell turnover zipo sawasawa kabisa ( Cell Turnover ni kuondoka kwa cell zilizokufa na kuja cell mpya zinazokufanya uwe na ngozi nzuri)

Namna Ya Kupata Rangi Moja Mwilini Kwa Kutumia Vitu Vya Asili

  • Inayotunzwa

Ngozi yako inakuwa na afya nzuri pale tu unapoijali na kuitunza na hapa tunaongelea mentally na physically, kufanya mazoezi, kulala vizuri, kula na kunywa vyakula vinavyolinda ngozi lakini pia kuepuka misongo ya mawazo ambayo inaweza kuleta madhara katika ngozi yako.

Related posts

1 Comment

  1. Buy DMT Vape Pen Australia

    … [Trackback]

    […] Read More to that Topic: afroswagga.com/urembo/skin-goals-ni-ipi/ […]

Comments are closed.