SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Style Ya Nywele Ya Kidoti Inavyo Haribu Nywele Zako
Urembo

Style Ya Nywele Ya Kidoti Inavyo Haribu Nywele Zako 

Hii style imekuwa maarufu sana, ni style rahisi kuibana lakini pia ni style ambayo unaweza kwenda nayo popote iwe kazini, kwenye mitoko ya kawaida na sehemu nyingine mbalimbali. Kutokana na urahisi wake wa kubana na kuwa useful wengi wetu tunapenda kuitumia mara kwa mara, lakini tuna sahau kwamba style hii inaweza kuharibu nywele zetu.

Namna Ambavyo Style Ya Kidoti Inaharibu Nywele

  • Kukata Nywele

Kubana nywele zako kidoti kila siku au mara kwa mara kunaweza kusababisha kukatika kwa nywele, hii hutokana na kuzivuta nywele juu kila siku. Zinaweza kukatika chini pembeni lakini pia hata juu pale unapofungia nywele hasa kama unatumia vibanio vya mpira.

Namna Ambavyo Unaweza Kuondokana Na Kukatika Kwa Nywele Unapobana Kidoti

  • Usibane Nywele Zikiwa Nyevu ( Zimeloa)

Nywele zetu huwa dhaifu pale zinapokuwa zimeloa, ukizivuta na kuzibana zinaweza kukatika kwa urahisi, subiri mpaka zikikauka vyema ndipo uzibane.

  • Paka mafuta kabla hujazibana

Hii huzifanya nywele kuwa laini na kuteleza pale ambapo zinavutwa, badala ya kukatika zinaweza kuteleza hasa kwa zile ambazo ni laini zaidi au fupi.

  • Badilisha style ya nywele zako mara kwa mara

Style zipo nyingi mno kama ni mpenzi wa kubana basi hakikisha unabadilisha sehemu za kubana, unaweza kubana up and low do wakati mwingine jaribu loose styles.

  • Tumia Vibanio vya nguo

Achana na vibanio vya mpira tumia vibanio ambavyo vimetengenezwa kutumia nguo na vizuri ni vile ambavyo vimetengenezwa kwa kutumia fabric ya satin.

Related posts

4 Comments

  1. hk firearms

    … [Trackback]

    […] Find More on to that Topic: afroswagga.com/urembo/style-ya-nywele-ya-kidoti-inavyo-haribu-nywele-zako/ […]

  2. HoyleCohen

    … [Trackback]

    […] Information on that Topic: afroswagga.com/urembo/style-ya-nywele-ya-kidoti-inavyo-haribu-nywele-zako/ […]

  3. https://www.buoyhealth.com/blog/health/phenq-reviews

    … [Trackback]

    […] Find More Info here to that Topic: afroswagga.com/urembo/style-ya-nywele-ya-kidoti-inavyo-haribu-nywele-zako/ […]

  4. Medicijnen bestellen zonder recept bij Benu apotheek vervanger gevestigd in Amsterdam

    … [Trackback]

    […] Info on that Topic: afroswagga.com/urembo/style-ya-nywele-ya-kidoti-inavyo-haribu-nywele-zako/ […]

Comments are closed.