Moja ya brand ambazo tunazipenda sana kwa sasa kutoka Tanzania niย Style Your Soul Clothing Line, hii ni brand ya mavazi na inamilikiwa na kijana aitwae George Williams, Style Your Soul ipo tofauti na brand nyingi za mavazi za Tanzania, hii ipo kipekee na very modern.
Hivi karibuni tumeona wameleta kitu kipya ambacho kime catch attention yetu, tumesha zoea kuona hand bags, fanny pack, ankle bags wao wamekuja na Hip Bag ambayo hii inavaliwa kwenye hips, ni kama fanny pack japo hii haivaliwei kiunoni inavaliwa kwenye hips. Aina hii ya bags mara nyingi huvaliwa na wanajeshi
Pochi hizi ni za leather as unawezakuona kwenye picha, lakini pia zina mikanda ambayo inakuwezesha kufunga pochi yako kwenye paja na kiunoni, kwetu tumeona ni idea nzuri na unique maana sio brand nyingi zimetengeneza pochi za aina hii. Lakini pia inakufanya uwe free kutembea au kama unamizigo mingi mkononi hasa ukiwa unaenda shopping ni nzuri kuwekea pesa na simu. Pia ni ndogo vitu vichache vinaweza ku-fit inakuwa nyepesi na kukupa urahisi wa kutembea.
kitu ambacho tumeona ni miss kwetu ni kwamba unatakiwa uvae na only aina ya nguo za suruali, yaani pants, suruali au tight huwezi kuvalia skirt au gauni.
Well let us know your views je ni yay or nay?
Related posts
HOT TOPICS
We need to have some sort of bima ila for enjoyment. Yaani wanakata ka % ka mshahara kako unakua na card ukienda seโฆ https://t.co/W9oDoaN2YY
FollowSubscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…