SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Njia Ya Kuondokana Na Ukavu Wa Nywele
Urembo

Njia Ya Kuondokana Na Ukavu Wa Nywele 

Kama una nywele natural / za asili utakuwa unajua shida ya hizi nywele kukaa na unyevu au kuwa na mafuta wakati wote. Nywele zetu za kiswahili ni kavu na zinanyonya sana mafuta. Hii method inasaidia kuzipa nywele zako unyevu unaotakiwa.

Wengi tukishaosha nywele tunapaka tu mafuta basi na tunadhani zitaendelea kuwa nyevu,kama wewe ni mmoja wapo basi soma zaidi hapo chini.

Nini maana ya LOC, LOC ina simama kama

  • Liquid
  • Oil
  • Cream

Liquid – hapa unaweza kutumia leave in conditioner ou kutumia maji ya kawaida kwenye spray battle

Oil – Haya ni yale mafuta ya maji, inaweza kuwa mafuta ya nazi, mafuta ya mnyonyo etc

Cream – haya sasa ni yale mafuta mazito

  • Baada ya kulowesha nywele zako kwa maji au kupaka leave in conditioner,paka mafuta ya maji kwenye nywele zako, ukimaliza unamalizia kwa kupaka cream katika ncha ya nywele zako changanya na chana nywele vizuri.
  • Unaweza kufanya hivi kila unapo osha nywele zako au pale unapohisi nywele zako ni kavu.

Hii njia ni nzuri kwenye type zote za nywele ziwe nywle nzito au nyepesi,

Related posts