SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

The Skincare Ingredients You Should Never Use Together
Urembo

The Skincare Ingredients You Should Never Use Together 

Unaweza kuwa na vipodozi vya ngozi vingi lakini bado ukawa unapitia magumu kwa maana ngozi bado haileti matokeo, hii inatokana na sababu kadha wa kadha lakini moja kubwa ni kwamba unaweza ukawa unatumia vipodozi ambavyo ingredients (viungo) vyake vinakingana yaani haviingiliani kwaio badala ya kutibu tatizo unazidi kufanya liwe kubwa.

Je ni ingredients gani hazitakiwi kutumika kwa pamoja?

  • Retinol + Vitamin C

Retinol na vitamini C ni viungo vyangu viwili pendwa vya wakati wote. Vyote viwili vina nguvu sana, viungo hivi vinapigana na baktertia wanaoweza kusababisha chunusi, huongeza uzalishaji wa collagen, na kuang’aza ngozi.

Lakini, viungo hivi havichezi vizuri pamoja. Retinol hufanya kazi vizuri zaidi katika pH ya 5.5-6. Vitamini C (katika fomu safi ya asidi ya ascorbic) inahitaji pH ya 3.5 au chini. Unaona tatizo?

Ni gumu kuunda bidhaa katika pH ambayo itatosheleza vitamini C na retinol. Lakini, hiyo haimaanishi kuwa hazina maana pamoja (kuna bidhaa nyingi nzuri ambazo zina viungo vyote viwili). Bado zinafanya kazi lakini sio kwa full potential yake.

Endapo ungependa kutumia viungo hivi vyote viwili basi

  • Tumia viungo hivi kwa nyakati tofauti za siku au wiki.
  • Chagua bidhaa zinazotolewa kwa wakati. Hii ina maana kwamba retinol huwekwa kwenye capsule na kutolewa polepole kwenye ngozi kwa muda wa masaa kadhaa. Vitamini C hutolewa mara moja. Kwa hivyo, muda mrefu baada ya kufyonzwa, retinol bado inasukumwa kwenye ngozi yako, bila ya kuingiliana na viungo vingine na kudhuriana katika ufanyaji kazi.
  • Tumia aina nyingine ya vitamini C. mfano Magnesium ascorbyl palmitate, ina pH mojawapo ya 7-8.5, hivyo inaweza kuingiliana kwa urahisi na retinol, bila kuathiri ufanisi.

  • Retinol + AHAs/BHA

AHAs (glycolic and lactic acid) and BHA (salicylic acid) ni powerful exfoliants. Retinol (a form of vitamin A), ambazo zinaweza kuharakisha cellular turnover (that’s scientific lingo for speeding up your skin’s natural exfoliating process).

Viungo hivi vyote hukusaidia kuondoa seli za zamani, zilizofifia na zilizoharibika kwenye ngozi ya uso wako na kuzibadilisha na kuleta ngozi mpya, ang’avu na yenye afy, kutumia vyote kwa pamoja vinaweza kusababisha ngozi kuwa nyekundu na kupata irritation

Endapo kuna umuhimu wa kuzitumia zote kwa pamoja basi hakikisha unazitumia siku na wakati tofauti ila usizimix na kupaka kwa pamoja.

  • Retinol + Benzoyl Peroxide

Je! unajua kuwa retinol inaweza kutibu chunusi pia? Vivyo hivyo kwa Benzoyl Peroxide, Ina hatua ya kuchubua ambayo huweka pores safi na kuua bakteria wanaosababisha chunusi.

lakini Benzoyl Peroxide yenyewe ni kali sana. Ndiyo maana ni matibabu ya mwisho kutumika kwa kutoa chunusi tu. Ukitumia vyote kwa pamoja yaani Benzoyl Peroxide na Retinol inazidi kuwa kali. Tarajia kuwa mwekundu, kutokwa ngozi pamoja na miwasho, je ungependa ku take hii risk?

Tumia kimoja na acha kimoja au endapo ungependa kutumia vyote kwa pamoja basi tumia Benzoyl Peroxide kupaka moja kwa moja kwenye sehemu zenye chunusi na Retinol sehemu nyingine, usimix vyote kwa pamoja.

Related posts