SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Tips Za Kupata Ngozi Nzuri
Urembo

Tips Za Kupata Ngozi Nzuri 

Kupata ngozi nzuri yenye kuridhisha ni janga, na hii hutokana na maswala mbalimbali kama tunavyokula, ukuaji, tunavyovitumia na mengine mengi. Lakini unaweza kupata ngozi nzuri endapo tu utajaribu kufanya mambo haya manne;

  • Usitumie Bidhaa Za Ngozi Nyingi

Wengi wetu tuna hii tabia unatumia kipozi hiki hakijaanza kutoa matokeo unajaribu kingine au una product za ngozi nyingi na zote unazitumia kwa wakati mmoja ni lazima makemikali yataingiliana na kuharibu ngozi yako. Kuwa mvumilivu na kujaribu kutumia vipodozi vichache kwa wakati mpaka pale utakapopata matokeo.

  • Tumia cleanser sahihi kwa aina ya ngozi yako

Sio cleanser inafaa kwa kila aina ya ngozi, hakikisha unapoenda kununua unauliza inafaa kwa ngozi ya aina gani au google na kusoma maelekezo yaliyoandikwa kwenye product si kwasababu rafiki yako anatumia inamfaa basi na wewe itakufaa.

  • Tumia sunscreen bilakujali hali ya hewa

Wengi hudhani sunscreen hutumika kwenye jua tu, hapana sunscreen ni muhimu kwakila aina ya hali ya hewa lakini pia sio tu unapokuwa nje bali hata kama upo ndani hatakama una shuka kwenye gari unaingia ofisini hakuna jua hakuna joto hakikisha unapaka sunscreen

Umuhimu Wa Kupaka Sunscreen Katika Ngozi

  • Epuka kugusa uso wako

Hili jambo ni gumu sana lakini pia ni muhimu sana, jaribu sana kuepuka kugusa uso wako mara kwa mara, mikono yetu inashika sehemu na vitu vingi ambavyo vinaweza kuwa na bakteria ambao wanaweza kuharibu ngozi zetu.

jinsi ya kutunza ngozi kilasiku

Related posts