SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Tofauti Ya Lightening Na Brightening Katika Vipodozi
Urembo

Tofauti Ya Lightening Na Brightening Katika Vipodozi 

Kuna mkanganyiko mkubwa juu ya vipodozi vya ngozi ambavyo vinadai kuang’aza na / au kung’arisha ngozi, mara nyingi ikisoma katika maelekezo ya vipodozi hivi unaweza kukuta vimeandikwa lightening ( Kung’aza) Au Brightening ( Kung’arisha) hapa wengi huwa tunaona ni kitu kimoja lakini kumbe ni vitu viwili tofauti.

  • Tunapoongelea Lightening ( Kung’aza)

Tunaongelea kung’aza ngozi kuwa katika hali ya kawaida, hii ni kama pale unapopata makovu ya chunusi, ngozi kupigwa na jua n.k. Lengo la kuang’aza ngozi ni kufifisha madoa yasiyotakiwa na kuipa ngozi yako rangi yake ya asili.

  • Brightening ( Kung’arisha)

Bidhaa hizi husaidia kung’arisha ngozi zaidi, sio kubadilisha ngozi katika rangi yake ya asili bali kuipa rangi asili ya ngozi yako mng’ao unaovutia. Unaweza kuwa umekutana baadhi ya watu wakiwa na ngozi yenye mvuto inang’aa ileile ya asili bila kuwa mweupe basi hivi vipodozi vilivyo andikwa au vyenye ingredients hizi ndio kazi yake.

Note: Hizi zote mbili ni tofauti kabisa na kujichubua au skin whitening.

Related posts