SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Tumia Juisi Ya Karoti Kutoa mikunjo kwenye Ngozi
Skin Care

Tumia Juisi Ya Karoti Kutoa mikunjo kwenye Ngozi 

Mikunjo katika ngozi ni miongoni mwa matatizo yanayowakabili wanawake wengi. Tofauti na mikunjo ya uzee, mikunjo hii hutokana na kuchoka kwa ngozi kunakosababishwa na mambo mbalimbali.  Mikunjo katika ngozi ni miongoni mwa matatizo yanayowakabili wanawake wengi.Tofauti na mikunjo ya uzee, mikunjo hii hutokana na kuchoka kwa ngozi kunakosababishwa na mambo mablimbali.


Katika kupambana na tatizo hilo, zifuatazo ni njia mbalimbali zinazoweza kutumika kutatua tatizo hili.Unashauriwa  kumwona mtaalamu wa afya kwa ushauri zaidi wa matumizi ya njia hizo za asili kabla ya kuanza kutumia njia za asili kwani hata kama ni vipodozi asilia, haina maana kama ni salama kwa watu wote.


Unaweza kutumia viungo vinavyopatikana jikoni kwako kupambana na mikunjo katika ngozi. Baadhi ya viungo hivyo ni pamoja na:

 • Karoti

Tumia juisi ya karoti kwa kupaka katika ngozi yako, hasa katika maeneo yaliyoathirika.Karoti ina virutubisho muhimu kwa ngozi yako. Pia ina uwezo mkubwa wa kuondoa sumu ndani ya ngozi.
Si hivyo tu, karoti inaweza kuondoa kabisa tatizo la mikunjo yangozi hasa sehemu za pembeni ya macho, shingo na maeneo kama hayo.

 • Namna ya kufanya


Chukua karoti, saga kwenye mashine kisha kamua ili kupata juisi yake. Tumia pamba kupaka katika maeneo yaliyoathirika, fanya hivyo mara kwa mara, itakusaidia kupunguza ama kuondoa kabisa tatizo hilo.

Carrot Facemask Kwa Ajili Ya Kung’arisha Ngozi

 • Maziwa


Maziwa yana virutubisho vinavyochochea kunawiri kwa ngozi.  Pia yana chembechembe za ‘Alfa-Hydroxide Acid’ ambazo zina uwezo mkubwa kuondoa seli zilizokufa mwilini.Yote haya husaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa tatizo la mikunjo katika ngozi.Unachotakiwa kufanyaKuchukua maziwa kiasi na chovya pamba ndani yake, kisha paka maeneo yaliyoathirika.

 • Aloe Vera

Jeli ya Alovera ndiyo hasa inayotakiwa katika zoezi hili. Chukua jani lake na kisha likate ili kupata utomvu wake.Chukua utomvu au jeli hiyo kama wengine wanavyoita na kisha pakaa sehemu iliyoathirika, itapunguza ama kuondoa kabisa tatizo hilo.

©binturembo 

Related posts

2 Comments

 1. แทงบอล betclic88

  … [Trackback]

  […] Read More Info here on that Topic: afroswagga.com/urembo/tumia-juisi-ya-karoti-kutoa-mikunjo-kwenye-ngozi/ […]

 2. qsymia weight loss stories​

  … [Trackback]

  […] Find More on that Topic: afroswagga.com/urembo/tumia-juisi-ya-karoti-kutoa-mikunjo-kwenye-ngozi/ […]

Comments are closed.