Tulio wengi tumezoea kutumia vipodozi mbalimbali vitengenezwavyo viwandani, Leo katika toleo hili maalum nataka tuangalie namna ambavyo tunaweza hudumia na kuitunza ngozi kwa kutumia viungo vya asili, nataka tuangalie ni namna gan mtu anaweza kutmia tende na limao/chungwa katika kutengeneza barakoa (mask) ya usoni.

  • Katika kutengeeza barakoa hii tunahitajivitu viwili, ambavyo ni Tende

tendeHapa tunaweza anza kuziandaa tende zetu, tunahitaji tende tisa au nane kwa barakoa tunaanza na kuzitoa kokwa/mbegu tu, hatuna haja ya kuzimenya

  • Lakini pia tutahitaji Limao/Chungwa

limaoTunahitaji nusu kipande tu ya limao letu kukamilishwa barakoa hii.

NINI CHA KUFANYA?

  • Kamua kipande cha limao na kupata juisi yake
  • Changanya mchanganyiko wa tende na juisi ya limao kisha tia kwenye kisagio, na usage
  • Osha uso wako au hakikisha uso wako ni msafi, paka mchangayiko wako usoni kisha usugue kwa vidole vyako na uuache kwa muda wa dk 10
  • Osha uso wako kwa maji ya baridi, kaushauso wako kwa kitambaa
  • Furahia muonekano mpya wa ngozi yako