SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Acha Kuhifadhi Perfume Sehemu Hizi Inapoteza Ubora
Urembo

Acha Kuhifadhi Perfume Sehemu Hizi Inapoteza Ubora 

Inawezekana umenunua unyunyu wako bei ghali kabisa na unaupenda sana lakini kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo ubora wa unyunyu wako unapungua na kukufanya ujiulize kwanini inatokea hivi? Inawezekana ukabadilika harufu sio yote lakini isiwe kama mwanzo au kutokukaa muda mrefu katika mwili kama zamani.

Utajiuliza kwanini hali hii imetokea? utaanza kuwaza labda umeuziwa perfume fake lakini kumbe inawezekana ni sehemu unayo hifadhi perfume yako ndio inasababisha yote haya, Je ni sehemu gani usihifadhi unyunyu wako na kwanini?

  • Weka Chupa za Perfume Mbali na Jua

Chupa za manukato nyingi hutengenezwa kwa glasi hivyo ukiweka manukato yako ambapo jua linapiga moja kwa moja (dirishani, dressing table iliyotazamana na mlango au dirisha) inaweza kuharibu haraka manukano, jua linaweza kusababisha joto ndani ya chupa ikapata mvuke na maji maji na quality ya manukato ikapungua. Hakikisha una hifadhi manukano yako sehemu yenye giza.

  • Weka Manukato Yako Mbali Na Joto

Basi kukwambia uweke manukato yako gizani sio ndio uweke kwenye kabati ufungie na milango kabisa, hapana. Joto jingi linaweza kuharibu kemikali zilizopo katika perfume na kupunguza ubora wake, hakikisha sehemu unayoweka ina hali nzuri sio joto kali kama ni kabatini au dressing table iwe sehemu ambayo haifikiwi na jua na pia ina ubaridi.

  • Weka Perfume Mbali na Unyevu

Wengi wetu huwa tunahifadhi manukato bafuni, ambapo hutumiwa mara nyingi. Kwa bahati mbaya, unyevu kupita kiasi unaweza kuharibu manukato, na wakati umwagaji au kuoga kwa kutumia maji ya moto katika bafu ni mbaya kwa manukato. Kwa kweli, hata vipodozi vilivyohifadhiwa katika bafuni yenye unyevu pia huvunjika kwa haraka zaidi. Hifadhi kipodozi bafuni endapo tu ni bafu lenye uwezo wa kutoa mvuke nje kwa haraka.

Related posts