SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Umuhimu Wa Kusoma Lebo Katika Vipodozi
Urembo

Umuhimu Wa Kusoma Lebo Katika Vipodozi 

Wengi wetu tunatumia vipodozi mbalimbali katika ngozi zetu, iwe kwa kuondoa kitu fulani au kukifanya kiwe bora zaidi. Imezoeleka kuwatunanunua vipodozi hivi kwa mazoea iwe kwa kuambiwa au kushauriwa na dakitari.

Mara nyingi huwa tunasahau kusoma lebo na kuona hakuna umuhimu kwa sababu tu kipodozi hiko kimemsaidia fulani au umeshauriwa na mtaalam basi hakina madhara, ni muhimu kusoma lebo ili kujua mambo yafuatayo:

 • Kujua Viungo / Ingredients zilizopo katika kipodozi hiko

Ni muhimu kujua kipodozi unachokipaka kina viungo gani na kama ni salama kwa ngozi yako, kwenye vipodozi huwa wanaweka kemikali mbalimbali na nyingine ni kali zinaweza kukusababishia madhara mbeleni. Oh yes inawezekana tusiwe wazuri sana kwenye haya mambo ya kusoma kuhusu kemikali kuna google jaribu ku-google na uone maelezo ya ingredient husika.

Fahamu Vipodozi Vitakavyo Haribu Mwili Wako

 • Expiry Date

Ni muhimu kujua kipodozi chako kinaisha muda wake wa kutumika lini, baada ya muda wa kipodozi kuisha inawezekana kisilete matokeo mazuri au pia kukuletea madhara katika ngozi yako.

Mambo Manne (4) Kuhusu Urembo Unapaswa Kujua

 • Namna ya kukihifadhi kipodozi chako

Kwenye label huwa kunamaelezo ya namna kipodozi chako kinafaa kuhifadhiwa, unaweza kuambiwa kisikae juani, kiwekwe sehemu ambapo joto lake ni kiasi fulani, ni muhimu kujua haya yote ili kupata matokeo mazuri ya kipodozi katika ngozi yako.

 • Namna ya kukitumia

Kwenye lebo kuna maelezo kama unaweza kukuta kimeandikwa kitumiwe mara mbili kwa siku asubuhi na wakati wa kulala, vingine havitakiwi kulala navyo, lakini pia kuna ambavyo unaambiwa utumie direct kwenye tatizo kama upake kwenye chunusi au doa tu bila kupaka kwingine ambapo hakuna madhara. Ni muhimu kujua haya yote.

 • Msimu wa kupaka kipodozi chako

Kuna vipodozi huwa vinapakwa kwa msimu labda wakati wa baridi au joto, inabidi ujue kipodozi unacho kitumia kinafaa kutumika katika msimu au hali gani ya hewa, japo si product nyingi ambazo huandikwa lakini unaweza kujua kwa kusoma ingredients zilizopo na zinafaa kutumiwa katika hali ipi.

VIPODOZI GANI UVAE KATIKA MSIMU HUU WA BARIDI (KIPUPWE)

Related posts

2 Comments

 1. mp3juices

  … [Trackback]

  […] Read More to that Topic: afroswagga.com/urembo/umuhimu-wa-kusoma-lebo-katika-vipodozi/ […]

 2. 예능 다시보기

  … [Trackback]

  […] Here you will find 7768 additional Info on that Topic: afroswagga.com/urembo/umuhimu-wa-kusoma-lebo-katika-vipodozi/ […]

Comments are closed.