Tunapoenda kwenye maduka ya vipodozi kununua vipodozi muuzaji atakwambia tu hiki kizuri kinafaa kwa ngozi yako, unakinunua na moja kwa moja unaanza kukitumia bila ya kusoma maelekezo yake ni vipi kinatakiwa kupakwa.
Ndani ya box la vipodozi kunakuwa na karatasi ambayo inatoa maelekezo yote ya kipodozi kimewekwa nini na kinafaa kupakwaje hii ni muhimu sana kuisoma,
Mfano mzuri ni juzi nilianza kutumia kipodozi kipya nilipewa maelekezo yote dukani lakini nilipofika nyumbani nikasema ngoja nisome “it won’t kill me kukipitia right?” nikasoma katika vyote muuzaji alivyonielekeza alisahau kuniambia kipodozi hiki hakifai kupakwa kama umetumia steam usoni na pia kama unakuwa exposed direct na jua.
Kama mtu ambae mara nyingi unatembea juani halafu ukapaka kipodozi ambacho hakifai kukaa nacho juani unaweza kubabuka au kuharibika ngozi, au ni mtu wa kufanya steaming uso ukafanya then ukapaka kipodozi hiki kunauwezekano mkubwa wa kupata madhara
Well let this set as a reminder kuwa mnasoma instructions kwenye vipodozi
Related posts
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…