SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Vitamin C Serum 101
Urembo

Vitamin C Serum 101 

Inawezekana umeshakutana nazo sana zikiwa zinauzwa kwenye mitandao au madukani, inawezekana umeshanunua na kuanza kuzitumia au unawaza kuzinunua. Wengi huwa wanatuambia faida zake na namna zinavyofanya kazi kwenye ngozi.

Lakini Je Vitamin C serum ni nini? zinafaa kwa ngozi ya aina gani? faida zake ni nini na je zinamadhara au ni faida tupu na je ni nini uangalie kabla ya kununua product hizi? haya yote utayajua hapa ambapo tutaongelea zaidi kuhusu product hizi:

Vitamin C Serum ni bidhaa ya ngozi ambayo ndani yake imekuwa packed na vitami , hii inaweza kuwa kwenye mfumo wa gel au liquid. Faida au jambo kubwa ambalo Vitamin C inayo ni antioxidant hivyo husaidia kuzuia kujitengeneza kwa free radical ambazo hupelekea au kusababisha uharibifu kwenye ngozi.

  • Antioxidant – ni compounds ambazo husaidia kudhibiti oxidizing agents kwenye living organism
  • Free Radical – ni particles ambazo zinajulikana kwa kuharibu cell afya katika miili yetu.

Utafiti Nyuma Ya Vitamin C Serum

Inawezekana kupata vitamin c kupitia vyakula na matunda aina mbalimbali kama machungwa, nanani,broccoli na mengine mengi, Vitamin C ni nutrient muhimu sio tu kwenye ngozi zetu bali pia katika ukuaji na maendeleo ya afya na miili yetu.

Vitamin C sio tu hupatikana kwenye kula bali pia inaweza kupatikana kwa kupaka mwilini na hapa ndipo Vitamin C serum inapoingia, Vitamin C hii ya kupaka hutengenezwa na si ya asili kama zile ambazo hupatikana kwenye chakula.

Je Nani Anafaa Kutumia Vitamin C

Kutokana na study, Vitamin C serum zinaweza kusaidia matatizo mbalimbali ya ngozi kama kuungua kwa jua, mikunjo, sagging, ukavu wa ngozi na kuwa na rangi mbili za ngozi, kama una matatizo haya ya ngozi basi unafaa kutumia Vitamin C kwenye ngozi yako. Lakini pia sio lazima uwe umefikia tatizo ndio uweze kuitumia bali unaweza kuanza kuitumia kabla ya tatizo ili kulizuia tatizo kama ambavyo waswahili husema “kinga ni bora kuliko tiba”

Vitamin C serum inaweza kutumika kwa watu wenye umri wowote hasa kuanzia miaka 18 ambao wapo kwenye nafasi kubwa ya kuwa wanakaa sana juani, lakini hii haimaanishi uache kutumia Sun Screen Cream unaweza kutumia vyote kwa matokeo bora zaidi.

Je Unawezaje Kuchagua High Quality Vitamin C Serum?

Vitamin C Serum zipo katika quality mbalimbali na bei pia hubadilika kutokana na quality, lakini pia unaweza kuuziwa yenye quality ndogo kwa bei kubwa, utajuaje quality hii ni ndogo au kubwa? Vitamin C Concentrate (ambazo kawaida huwa zinakuwa referred kama L-ascorbic acid or ascorbic acid kwenye Label ya product) , kuna ambazo zinakuwa na percent 10,15 mpaka 20, Vitamin C Serum nzuri ni ile yenye L-ascorbic acid au Ascorbic Acid yenye percent kuanzia 8 chini ya hapo ni low quality. Study inasema the higher the concentration the stronger the serum.

Kwa leo tunaishia hapa tukutane kwenye sehemu ya pili ambapo tutajua Faida, Namna ya kutumia kupata matokeo mazuri na madhara yake kama yapo.

Related posts