SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

VITU 7 KUTOKA JIKONI VINAVYO WEZA KUSAIDIA UKUAJI WA NYWELE ZAKO
Dondoo

VITU 7 KUTOKA JIKONI VINAVYO WEZA KUSAIDIA UKUAJI WA NYWELE ZAKO 

Bidhaa za urembo hasa wa nywele na ngozi vina panda bei siku by siku yaani day and night, leo una weza kuta elfu ishirini ukaenda kesho ukaambiwa elfu thelasini, basi ili mradi tafrani na hii ina tokana na demand ya vitu hivi kuwa kubwa. Kwa sasa kila mwana dada ana taka awe na ngozi nyororo na nywele kama za Priyanka Chopra.

Kwa wenzetu na sie wasio kuwa nacho au tunacho lakini wabahili kweli kabisa nitoe 40,000 kwa ajili ya nywele? hapo si nina nguo zaidi ya thelasini mwenge lol wengi wetu ndivyo tusemavyo. Lakini hata kama una hela vitu vya asili ni vizuri zaidi na vina manufaa mengi zaidi basi na hivi ni vichache vinavyo weza kusaidia ukuaji wa nywele zako, vipo tu jikoni mwako labda hukuwa unajua basi ngoja tuku habarishe

  • Juice ya kitunguu -Kitunguu kina sulphur ambayo husaidia ku ongeza ufanisi wa tissue ambazo zinaweza kusaidia ukuaji wa nywele zako, kata kipande cha kitunguu paka katika ngozi ya kichwa chako kaa nayo kwa dakika 15, kisha osha na shampoo

  • mask ya yai- yai (mayai) yana sifika kuwa na protein nyingi ambazo zina weza kusaidia ukuaji wa nywele, namna ya kufanya ni rahisi tenganisha ute wa yai na kiiti cha yai kisha ule ute ongezea na kijiko cha chai cha mafuta ya oilve oil na asali, changanya mchanganyiko wako vizuri kisha paka katika ngozi ya kichwa chako kaa nayo kwa muda wa dakika 20, osha kwa maji ya baridi na shampoo kuondoa harufu.

  • Olive oil -kukuza na kuzipa nywele zako unyevu olive oil are the best, weka nusu kikombe ya mafuta ya olive oil kisha yapashe moto na uyaache ya poe yasiwe ya moto sana walabaridi yawe ya uvugu vugu. Paka na lowesha nywele zako kwa mafuta hayo vaa mfuko wa plastick kaa nao kwa muda wa lisaa limoja kisha osha na shampoo.

Baking soda: chukua vijiko vwili vya baking soda na dilute na vikombe vitatu vya maji, baada ya kuosha nywele zako na shampoo kabla ya ku conditioner osha na maji ya baking soda, kisha endelea na kufanya conditioner.

green Tea: Green tea ina saidia ku boost ukuaji wa nywele pia kupunguza ukatikaji wa nywele, green tea ina sifika kuwa tajiri wa antioxidant ambayo inasaidia kukuza nywele zako efficiently, paka maji ya uvuguvugu green tea kwenye ngozi ya kichwa chako kaa nayo kwa lisaa limoja kisha osha.

Apple Cider Vinegar: apple cider vinegar ina saidia vitu vingi kuanzia nywele, ngozi hadi kupunguza uzito lakini kwa leo tunaongelea nywele unacho takiwa kufanya ni, dilute apple cider vinegar yako kwa kumix 15ml ya apple cider vinegar na vikombe viwili vya maji, shake it well kisha baada ya kuosha nywele zako na shampoo na conditioner osha na maji ya apple sider vinager

Tui la nazi – tui la nazi lina sifika kwa kuwa na madini ya chuma,potassium na fat kwa wingi, ni nzuri kwa ukuaji wa nywele unacho takiwa kufanya ni kupata tui la nazi na kipande cha limao changanya pamoja kisha paka katika ngozi ya kichwa chako, iache kwa muda wa masaa ma 4-5 kisha osha

 

Related posts

3 Comments

  1. Liberty Caps Mushroom

    … [Trackback]

    […] Find More here to that Topic: afroswagga.com/urembo/vitu-7-kutoka-jikoni-vinavyo-weza-kusaidia-ukuaji-wa-nywele-zako/ […]

  2. pay off credit card debt

    … [Trackback]

    […] Info to that Topic: afroswagga.com/urembo/vitu-7-kutoka-jikoni-vinavyo-weza-kusaidia-ukuaji-wa-nywele-zako/ […]

  3. Bubble Tea

    … [Trackback]

    […] Read More on that Topic: afroswagga.com/urembo/vitu-7-kutoka-jikoni-vinavyo-weza-kusaidia-ukuaji-wa-nywele-zako/ […]

Leave a Reply