SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Vitu Unavyoweza Kufanya Weekend Vikasababisha Skin Breakout
Urembo

Vitu Unavyoweza Kufanya Weekend Vikasababisha Skin Breakout 

Umeshawahi kuwa na ngozi nzuri week nzima kisha unaanza jumatatu yako na ngozi ambayo huelewi? unaanza kujiuliza hizi rashes nimetoa wapi au mbona ngozi yangu imeharibika ghafla? Hii hutokana na mambo kadhaa ambayo tunayafanya weekend na yanaweza kuwa chanzo cha skin breakout

  • Kuto Kulala Kwa Masaa 8-9

Tunajua kutokupata usingizi wa kutosha kunaweza kuzidisha kuonekana kwa aging signs na kupunguza skin elastic ambayo itapelekea kuzidi kuonekana kwa makunyanzi ya ngozi pamoja na uneven skin pigmentation. So jaribu kupata usingizi wa kutosha na usiangalie Tamthilia au kukesha weekend nzima

  • Kula Junk Food

Weekend tunatoka tunaenda ku-enjoy maisha unaweza kujikuta siku nzima umekula un-healthy food zenye mafuta au sukari nyingi, hii inaweza kupelekea kusababisha chunusi usoni, hakikisha una kula vyakula vya aina hii kwa kiasi usizidishe.

  • Kulala Na Makeup

Inawezekana umetoka na marafiki ukapaka makeup yako umerudi umechoka unaamua kulala nazo hivyohivyo, hii pia inaweza kupelekea upate skin breakout, hakikisha ukirudi unaondoa makeup yako kisha ulale.

  • Kuacha Nywele Zikagusa Uso Wako

Weekend tunajiachia unaenda kutengeneza nywele unaziachi, umepakwa mafuta ya nywele zinagusa uso wako zile kemikali zilizopo kwenye vipodozi vya vywele vinaingia kwenye ngozi yako na kuleta madhara, hakikisha style ya nywele unayoiweka hata kama ni ya kuziachia sio kubana basi nywele hazigusi uso.

  • Kuto Kupaka Sunscreen

Inawezekana unatoka au hutoki unahisi hauna haja ya kupaka sun screen, hakikisha ukitoka au usipotoka hata kama upo ndani unapaka suncreen yako ili kukuepusha na breakouts.

Tuwatakie weekend njema na jitahidi kulinda ngozi yako

Related posts