SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Vyakula Vya Kuepuka Kama una Ngozi Ya Mafuta
Habari

Vyakula Vya Kuepuka Kama una Ngozi Ya Mafuta 

Kuna msemo unaosema “you are what you eat”, yes huu msemo hauja kosea kama ambavyo inajulikana ukila vyakula vya ajabu ajabu vina haribu mwili wako basi ni sawasawa na ngozi hasa ngozi ya mafuta, sio tu vinazidi kufanya ngozi yako kuwa na mafuta lakini pia zinaweza kusababisha matatizo ya ngozi kama chunusi,white heads na black heads etc. Lakini habari nzuri ni kwamba unaweza kuepuka haya yote kama utaondoa baadhi ya vyakula katika diet yako, well waswahili husema “mtaka cha uvunguni shurti uiname” kama unahitaji kitu inatakiwa ukubali ku strive for it.

leo tunawaletea baadhi ya vyakula ambavyo unatakiwa kukaa mbali navyo kama ngozi yako ni ya mafuta

Vyakula Venye/ Vilivyo Tengenezwa Na Maziwa Mengi

Vinaweza vikawa ni vyakula vyako pendwa au vinaulazima kutumika katika maandalizi ya chakula lakini tuamini hivi vyakula vina matokeo makubwa ambayo yanaongeza mafuta katika ngozi yako, unaweza kupunguza au kuacha kabisa kutumia vyakula kama Ice cream, butter,butter milk etc.

Kahawa Au Chai

Kahawa na chai vina dyhdrate mwili wako hii inaweza kupelekea uzalishaji wa mafuta na kusababisha chunusi na vipele vidogo vidogo, unaweza kupunguza kunywa chai na kahawa na kunywa maji mengi na handmade juice.

Pombe

Pombe ni kama kahawa ina dydrate mwili wako ambapo inaweza kupelekea uzalishaji wa mafuta mwilini na kusababisha ngozi kuendelea kuwa na mafuta lakini pia kupata skin issue kama chunusi.

Sukari

Kutumia sukari husababisha spike katika blood sugar levels. Hii inaongoza kwa uzalishaji wa insulini zaidi, ambayo, kwa upande wake, husababisha tezi za kuzalisha mafuta zaidi. Hii inapelekea kuwa na  ngozi yenye mafuta ambayo matokeo yake huleta chunusi . Epuka  kula mikate,  jamu, vyakula vya unga, na pipi. Tumia sukari za asili, zilizopo katika matunda na mboga, kwa kiasi.

chumvi

Chumvi ya ziada inaweza kusababisha uhifadhi wa maji na kuvimba. Inaweza pia kusababisha ongezeko la oil levels katika ngozi, pale ambapo mwili unapo jaribu kupambana na  maji machafu yanayosababishwa kutokana na matumizi makubwa ya chumvi. Epuka kula chumvi ya ziada au vyakula vyenye chumvi nyingi.

 

Related posts

3 Comments

  1. official website

    … [Trackback]

    […] Info on that Topic: afroswagga.com/urembo/vyakula-vya-kuepuka-kama-una-ngozi-ya-mafuta/ […]

  2. Residual income

    … [Trackback]

    […] Information to that Topic: afroswagga.com/urembo/vyakula-vya-kuepuka-kama-una-ngozi-ya-mafuta/ […]

  3. psilocybin mushrooms for sale colorado

    … [Trackback]

    […] Find More Info here on that Topic: afroswagga.com/urembo/vyakula-vya-kuepuka-kama-una-ngozi-ya-mafuta/ […]

Comments are closed.