Make Up ni urembo unakuja kwa kasi sana duniani, kila mtu ana taka kujua kupaka make up, wengine wana taka kujua kwa ajili ya matumizi ya binafsi na wengine wana taka kwa ajili ya biashara.
Ni kawaida kwa kila mwanamke kutaka kuonekana mrembo kuliko mwingine iwe naturally au kwa kupaka make up. Lakini hii make up imachukua nafasi kubwa Zaidi maana ina ongeza uzuri wa muonekano wako wa kawaida kuna wengine ukiwaona kabla na baada ya kupaka make up unaweza ukamsahau. Make up inafanya watu wasahau au kuto kupenda mionekano yao ya kawaida, una fanya watu wasijali ngozi zao kwa sababu tu ana weza kuziba chunusi kwa kupaka make up.
Ni wanawake wachache sana hivi sasa ambao wana confidence ya kutoka nyumbani bila ya kupaka make up. Kuna baadhi ya wambaji wa make up ambao wana weza kukubadilisha kuwa mtu yoyote unae taka kua ki sura, hii ufanya watu wote tufanane duniani.
Ukiuliza wanawake kwanini wana vaa make up huto pata jibu moja wengine husema wana paka make up wawe wazuri,wengine kujiamini, wengine kuonekana vijana lakini ukweli kuna ambao wasipo paka make up wana onekana wazuri na vijana kuliko wakipaka make up.
Imekua kawaida sasa kukutana na mwanamke kapaka make up bila ya kuwa na mahala popote muhimu pa kwenda wakati inaaminika make up ni urembo upakwao pale unapo kuwa na sehemu muhimu ya kwenda kama sherehe za harusi,kupokea tuzo na matamasha mbalimbali. Na kibaya Zaidi wengi wao hawatambui aina na nyakati za kuvaa make up.
Wengi hutumia kipato chao kidogo wakipatacho katika manunuzi na matumizi ya make up na kusahau mambo mengi ya faida Zaidi kuliko make up. Si vibaya kupaka make up au kununua lakini ni vizuri kujua nyakati na kutumia kipato kidogo katika kuwekeza kwenye vipodozi hivi.
Related posts
2 Comments
Leave a Reply Cancel reply
You must be logged in to post a comment.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Info on that Topic: afroswagga.com/urembo/wanawake-wa-kisasa-na-make-up/ […]
… [Trackback]
[…] Find More on on that Topic: afroswagga.com/urembo/wanawake-wa-kisasa-na-make-up/ […]