SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Wapi Unaweza Kupata BidhaaVipodozi Vya Asili Tanzania
Urembo

Wapi Unaweza Kupata BidhaaVipodozi Vya Asili Tanzania 

Kama ni mpenzi wa bidhaa za asili za urembo utagundua kwamba ni kazi sana kupata bidhaa hizi, madukani kumejaa bidhaa za urembo zenye makemikali. Na ukifanikiwa kupata sehemu ambayo inauza vitu vya asili huwa ni ghali kutokana na kwamba wananunua kutoka Nje. Lakini katika kufanya research zetu tukagundua kwamba kuna mwanadada ambae ana tengeneza bidhaa za asili kutoka Tanzania na ana kila ktu, kuanzia mafuta ya ngozi na nywele, sabuni, scrub,lip balms na hata clay’s  ambazo huwa ni shida sana kupata anaitwa Hellen Dausen ambae ni mmiliki wa kampuni ya Nuya Essence

Tulisha fanya nae interview unaweza kusoma kwa kubonyeza link hapo juu lakini katika maswali ambayo tulimuuliza moja wapo muhimu lilikuwa kwanini aliamua kuanzisha biashara ya urembo wa asili?

Afroswagga – katika ulimwengu huu wa kujichubua nini kilikuvuta mpaka kuanzisha biashara ya natural.

Nuya -Nimeona wanawake wengi wakihudhurika sana na hii mikorogo, na hivo ikanilazimu kuwa natoa mafunzo na kuwaelekeza jinsi ya kutunza ngozi zao na zikapata ung’aavu mzuri ambao ni zaidi ya kuwa hata mweupe. Na pia kuwaelimisha madhara ya madawa haya makali. Na hivo ikawa kama mvuto wa ziada kwa kazi yangu. 

 

Lakini je huwa ana wafikiria watu wenye matatizo ya ngozi?

Afroswagga – katika kutengeneza product zako huwa una fikiria watu wenye matatizo ya ngozi labda akitumia mafuta ya nazi ana haribika ngozi na una kabiliana nayo vipi ili kuweza kuwasaidia?

Nuya – Kwa kweli kila mtu ana ngozi tofauti na kweli kuna wateja wachache ambao mafuta ya nazi ngozi zao hazikubali kabisa japo ni natural, kwa hiyo tuna mafuta mengi mengine ambayo mteja anaweza kujaribu na ikawa sawa kwa ngozi yake. Tunaelewa kuwa kuna watu watakuwa na allergy na mafuta kadhaa na hivo tunajaribu kuleta mafuta ya aina mbali mbali ili aina moja ikiwa haifanyi kazi vizuri basi anaweza kujaribu mafuta mengine mpaka akapata yale yanayompenda. Ukiangalia sabuni zeti zimeandikwa zinasaidia matatizo ya ngozi Fulani, kama Charcoal soap, husaidia ngozi ya mafuta, Goat Milk soap, husaidia ngozi kavu….ndio, huwa nafikiria product ninayotengeneza itasaidia ngozi aina gani.

 

Sisi kama afroswagga tunaweza kusema ni ma ambassador wa kushauri watu kutumia bidhaa za asili na hii ni kutokana na kwamba bidhaa zenye kemikali zina madhara mbalimbali ikiwepo kuharibu ngozi lakini pia magonjwa, lakini vipodozi vya asili vinatumika mara nyingi katika vitu tofauti tofauti kama mafuta ya nazi unaweza kutumia katika nywele lakini pia ngozi hivyo ina punguza gharama.

Wanamaduka yao DAR  na Zanzibar * STONE TOWN * NUNGWI, lakini pia kama upo nje ya sehemu hizi wana safirisha, unaweza kuwafollow Instagram@nuyasessence na katika blog yao  nuyasessence.com

Ni matumaini yetu tumekusaidia kujua wapi unaweza kupata vipodozi vyako vya asili.

 

Related posts