Inawezekana ukawa una paka makeup kwa urembo, inawezekana wewe ni mpakaji makeup (make up artist) ambae ulivutiwa tu kwa kuona wengine wanafanya lakini ukiulizwa nini maana ya makeup na ina faida gani huwezi kujibu well tupo wengi, sana sana jibu letu litakuwa kumfanya mtu azidi kuonekana mrembo ambalo ni kweli lakini kuna faida nyingine nyingi zinazo tokana na makeup.

Makeup – ni cosmetics / urembo ambao una tumika kuremba uso na kuufanya unekane vizuri zaidi. Vitu kama Mascara, Lipstick na eye shadow kwa ujumla vinaitwa makeup

Je make up zina faida gani ukiachana na kuremba uso

  • Kupunguza miwasho ya ngozi – makeup hutengenezwa na kemikali mbalimbali lakini ndani yake zipo ambazo zinaweza kusaidia kutunza ngozi yako, kama kuipa unyevu na kusaidia ngozi isikauke na kukuwasha.
  • Kupunguza mikunjo ya sura – hii inawezekana kila mtu anaijua kama ni mpenzi wa urembo unaweza ukawa umesha ona hata kwenye mitandao jinsi ambavyo make up artist wanawapaka make up wazee ambao baada ya kupakwa huonekana kama vijana, lakini ukiachana na hilo pia kemikali zitumikazo nyingine zinasaidia kufanya ngozi kuwa laini na kupunguza mikunjo.

  • Sun Protection – unapo paka makeup jua likipiga haligusi ngozi linakutana na layer za makeup na kuishia hukohuko hii inasaidia ngozi yako kuto kupigwa na jua na kupata vipele au kuwa mweusi.
  • Inazuia Break outs (kuharibika kwa uso) – kuna makeup ambazo ndani yake zinakemikali ambazo husaidia kuondoa chunusi unacho takiwa kufanya ni kusoma maelezo ya aina ya make up unayo nunua ina vitu gani ndani yake, unapo kosea kununua makeup ambayo haiendani na ngozi yako zinaweza kuleta matokeo hasi pia.

Comments

comments