Unapochagua mascara kuna mambo muhimu ya kuzingatia kulingana na lengo lako unalotaka kutimiza. Unatakiwa kujua unataka kope zionekane ndefu( lengthenning), zionekane zimejaa/nene (thickenning), zisishikane na je ukinawa na maji mascara itoke au laa (water proof).
Wengi tunanunua tu mascara kwa wamachinga nk bila kujua itafanya nini mradi ukipaka kope zinaonekana.
Ya Kurefusha kope( lengthenning)
Hii kibrashi chake kina vinyweleo vingi ili ifikishe mascara vizuri kwenye kope hasa katika ncha za kope, Urefu wa kope hutengenezwa na namna mascara inavofika vizuri kwenye ncha (tips) za kope. Unapopaka mascara katika kope hakikisha ncha za kope umezifikia vizuri.
Unaweza usibandike kope za bandia lakini mascara ikakubeba ukaonekana na kope ndefu.
Ya kujaza kope (thickener)
Hii huwa na kibrashi ambacho ni rahisi kufikisha mascara katika shina la kope zako kuzipa ujazo. Na pia unaweza kuzifanya zijae kwa kuziviringisha katika brashi yako. Hakikisha imeandikwa Volume/ thickener: mara nyingi zimetengenezwa na nta flani na kemikali aina ya silicone ambavyo hufanya kope kuwa zimejaa.
Mascara zisizojirundika na kunatisha kope
hii huwekwa viungo vya silk na glyserini pia kibrashi chake huwa kirefu na vinyweleo virefu ili mascara ikolee kwa kulingana katika kope. .
Waterproof Mascara
Hizi huwekwa viungo maalumu vinavyoweza kukinga unyevunyevu usiathiri kipodozi chako. Kwa hiyo mascara hii haivurugiki kirahisi ukipaka. Lakini saa nyingine viungo vyake huwa vina ukali hivyo ni vema ukapaka kope zako vaseline kabla ya kupaka ili kope zisikatike
Pamoja na yote hayo, Angalia bajeti yako iko vipi ili kujipatia unachoweza kumudu na ambacho kinatimiza lengo.
Inasemekana saa zingine sio kemikali tu za kwenye mascara bali pia aina ya kipakio chake huweza kuleta matokeo mazuri.
wingi wa vinyweleo vya brashi na urefu huamua urahisi katika upakaji wake, mfano ili uweze kupaka vizuri kwenye ncha za kope unahitaji brashi ndefu yenye vinyweleo vingi
Related posts
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…