SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Zijue Mbinu 9 Za Kuondoa Harufu Ya Kikwapa
Urembo

Zijue Mbinu 9 Za Kuondoa Harufu Ya Kikwapa 

VIJANA wanapofikia umri wa kubalehe, moja kati ya dalili wanazokumbana nazo ni kuota nywele sehemu za siri ikiwamo kwapani. Wengi wao wamekuwa wakishindwa kujiweka katika hali ya usafi hivyo kujikuta wakitoa harufu kali ya jasho. Jambo hilo huwakwaza watu wengi na hivyo kujikuta wakijitenga /wakitengwa bila kujua sababu.

Kunuka kikwapa  ni  tatizo kubwa katika mwili wa binadamu. Tatizo hili husababishwa na bakteria wanaovutiwa na jasho au unyevunyevu chini ya kwapa. Sasa basi, kuna njia nyingi ambazo watu wengi huzitumia ili kwapa liwe na harufu nzuri, kavu na safi. Zifuatazo ni mbinu 9 za kuondoa / kuzuia kikwapa

1.Wengine hutumia njia za kisasa ambazo ni pamoja na kupaka deodoranti au pafyumu zinazosaidia kuondoa harufu mbaya mwilini.

2. Lakini kama hiyo haitoshi, kuna njia za asili Kabisa  zinazoweza kuzuia harufu ya kwapa ambazo ni pamoja na kupaka kipande cha limao kwenye kwapa na kuacha lipate hewa  safi ili kuua vijidudu na kutoa tezi za jasho kuondoa harufu mbaya.

3.Kuvaa nguo safi zenye nyuzinyuzi za asili kama pamba, hariri na sufi zitasaidia kufyonza unyevu na kuliacha kwapa lako kuwa kavu, safi na bila harufu mbaya.

4. Kuoga kila siku na kusafisha nguo kwa maji safi kunasaidia kuua bakteria na ambao husababisha harufu mbaya.

5. Pia kunywa maji mengi kila siku kunakusaidia kutoa sumu mwilini na hivyo kupunguza harufu mbaya ya kwapa.

6. Njia nyingine inayoshauriwa ni kuhakikisha kuwa unaosha kwapa mara kwa mara kwa kutumia sabuni zenye dawa (medicated soaps).

7. Aidha, kupunguza kula chakula chenye viungo vingi hasa vitunguu. Inasemekana kuwa kula vitunguu vingi kunachangia mwili kutoa harufu kali.

Licha ya pafyumu na spray kusaidia kuondoa harufu mbaya mwilini, hii si dawa endelevu kwani baada ya muda harufu inaweza kurudi palepale hivyo ni vema kutumia njia za asili kukabiliana na hali hiyo. Pafyumu haiwezi kutibu tatizo moja kwa moja.

8.Pia inashauriwa kuwa baada ya kuoga jifute kwa taulo au kitambaa safi na usiache unyevu unyevu ambao huwavutia bakteria kukua katika maeneo yaliyojificha (yenye mikunjo).

9.Mbinu nyingine ni kujitahidi kunyoa nywele za kwapa mara kwa mara na kuepuka kukaa sehemu zenye joto kupita kiasi kwa muda mrefu.

Jee ni mbinu gani uliyokuwa ukiitumia hapo Kabla? Imeandikwa Na @binturembo

Related posts

3 Comments

 1. Order DMT online New South Wales

  … [Trackback]

  […] Find More on on that Topic: afroswagga.com/urembo/zijue-mbinu-9-za-kuondoa-harufu-ya-kikwapa/ […]

 2. penis prosthetic big penis big prosthetic big dildo erect penis prosthetic

  … [Trackback]

  […] Info on that Topic: afroswagga.com/urembo/zijue-mbinu-9-za-kuondoa-harufu-ya-kikwapa/ […]

 3. https://www.kirklandreporter.com/reviews/phenq-reviews-fake-or-legit-what-do-customers-say-important-warning-before-buy/

  … [Trackback]

  […] Find More to that Topic: afroswagga.com/urembo/zijue-mbinu-9-za-kuondoa-harufu-ya-kikwapa/ […]

Comments are closed.